Vera aanika mwili kwa kuvalia nguo iliyombana akiongoza tamasha mjini Kitale - Welcome to Topleveltz Entertainment and Music Website

Ads Top

Vera aanika mwili kwa kuvalia nguo iliyombana akiongoza tamasha mjini Kitale

Vera aanika mwili kwa kuvalia nguo iliyombana
Vera aanika mwili kwa kuvalia nguo iliyombana akiongoza tamasha mjini Kitale  

Malkia wa makalio Vera Sidika alisherehekea miaka 30 tangu kuzaliwa kwake Jumamatu, Septemba 30.
Kipusa huyo aliandaa tamasha la kukata na shoka katika klabu cha Epic mjini Kitale.

Kutokana na umaarufu wake, kipusa huyo aliwavutia watu wengi waliowasili eneo hilo la burudani kutokana na video aliyoipakia kwenye ukurasa wake wa Instagram. TUKO.co.ke imebani kwamba wamiliki wa klabu hicho walimwalika kipusa huyo na kumpa jukumu la kuendesha tamasha iliyoandaliwa Jumamosi, Septemba 28.

Tamasha hilo lililoitwa Vera Sidika Birthday Party lilihudhuriwa na watu wengi ambao walikuwa na tamaa ya kulisha macho.
Shosholaiti huyo aliwasili tayari kwa biashara huku akiwa amevalia vazi fupi jeusi lililombana na kufichua uzuri wa ngozi yake nyeupe na nyororo.

Baadhi ya waliohudhuria walijivinjari na kuanza kumuosha na hela kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, pesa ambazo alizisanya na kuanza kuzigawa miongoni mwa mashabiki hao. Baada ya hapo alisafiri hadi Tanzania ambapo alijumuika na mpenzi wake na familia yake


Loading...
Powered by Blogger.