Ads Top

NEWZ ALERT: WATU ZAIDI YA 60 WAPOTEZA MAISHA NA 60 WAJERUHIWA BAADA YA TANKI LA MAFUTA KULIPUKA MOTO MOROGORO.

Loading...
#UPDATESAJALIMORO : Hospitali ya Rufaa ya Morogoro  imethibitisha kupokea miili 60 na majeruhi 60.

 “…Tunavyoongea sasa hivi tumeshapokea majeruhi 60, na bado tunaendelea kupokea. Kati ya hao walio ndani ya ward wanaume ni 58 na wanawake ni wawili…na pia tumepokea miili 60,lakini bado hatujafika mwisho tunaendelea kupokea kutoka eneo la tukio, ” Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Morogoro, Rita Lyamuya.Ínaripotiwa kuwa Idadi kubwa ya watu wanahofiwa kuungua moto na kupoteza maisha baada ya tenka la mafuta kuwaka moto eneo Msamvu Itigi mkoani Morogoro asubuhi hii.Inadaiwa kuwa chanzo  ni watu kutaka kuiba betri kutoka kwenye tenka hio iliyokuwa imepinduka huku wengine wakiiba mafuta, ndipo moto ukalipuka. Juhudi za kuopoa miili zinaendelea.Aidha Mashuhuda wa tukio hilo wameviambia vyombo vya habari kuwa lori la mafuta (petroli) lilipinduka, hivyo watu mbalimbali, wengi wao wakiwa madereva wa pikipiki wakaenda eneo la tukio na vibebeo kwa lengo la kupata mafuta.Vyombo vya Ulinzi na Usalama vimekwishawasili eneo la tukio kwa ajili ya kutoa msaada kwa kadiri itakavyowezekana,ikiwemo na kubaini idadi ya watu waliopoteza maisha.MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI-AMENTUNAENDELEA KUSUBIRI TAARIFA RASMI KUTOKA KWA MAMLAKA HUSIKA.


NEWZ ALERT: WATU ZAIDI YA 60 WAPOTEZA MAISHA NA 60 WAJERUHIWA BAADA YA TANKI LA MAFUTA KULIPUKA MOTO MOROGORO.
Loading...

No comments:

hide

Powered by Blogger.